"Nikiwa kwenye mgahawa wa The Green Roof sehemu ambayo tulipenda kukutana mimi na Sonia, ninajaribu kumuangaza angazaa mara tu nilipofika hii ni baada ya kupokea ujumbe kuwa nataka tukutane pale. Haikuniwia ngumu kupata sehemu aliyokuwa kaketi pamoja na wingi wa watu uliokuwepo eneo hilo siku hiyo. Kutokana na yeye kuwa ameketi sehemu ambayo huwa tu"...