Fahamu zaidi kuhusu sisi
Sheria

Tunazingatia sheria za nchi na zile za uandishi wa hadithi na tamthilia katika kuandaa simulizi zetu, Pia tunazingatia umri na lika la wasikilizaji na wasomaji wa simulizi zetu, vile vile tunatumia majina ya kufikilika yasiyo walenga watu moja kwa moja katika jamii.

Lugha

Hadithi hizi pendwa zimeandaliwa katika lugha ya kiswahili ili kuwafikia watanzania wote ndani na nje ya mipaka yetu, pamoja na Afrika Mashariki yote, Kenya, Tanzania, Rwanda, Burundi na Uganda.

Fani

Tumebobea katika fani za utunzi na masimulizi ya tamthilia na hadithi mbalimbali zilizo jikita katika mazingira ya tamaduni za kiafrika na zile za kigeni.

Hisia

Tumelenga kugusa hisia za wasikilizaji na wasomaji katika mapenzi, maumivu makali ya moyo, Usaliti, Ukatili, Wivu, Chuki, Ukakamavu na Ujasili, Tamaa mbaya, Kunyanyapaa, Uvumilivu, Uhodari na Nguvu za giza(Uchawi) katika mazingira tofauti.